Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji Muongozo kwa Wanaoanza Ufugaji











>> YOUR LINK HERE: ___ http://youtube.com/watch?v=MLJxsyxuOwk

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji - Muongozo kwa Wanaoanza Ufugaji • Kuku wa kienyeji wakifugwa kwa kuzingatia taratibu na kanuni bora za ufugaji wa kuku, wanaweza kuwa chanzo cha mapato na kuinua kipato cha familia. Vilevile wanaweza kupunguza tatizo la lishe kwa kuzalisha mayai na nyama isiyokuwa na madhara. • SUBSCRIBE: https://bit.ly/2OvSiRm • Zifatazo ni hatua za ufugaji bora wa kuku wa kienyeji:- • 1. Kutafuta elimu ya ufugaji bora wa kuku, elimu ambayo itakusaidia kupunguza changamoto za magonjwa na vifo. • 2. Kuchagua Mfumo wa kufugia na Kujenga banda la kuku • Kati ya mifumo mitatu ya ufugaji wa kuku, mfumo wa huria au nusu ndani nusu nje ndio mifumo mizuri kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji. • 3. Chagua mbegu bora ya kufuga • Uchaguzi wa mbegu bora ni moja ya vitu vya kuzingatia kwenye kwenye ufugaji wa kuku. Kwenye kuku wa kienyeji nikisema mbegu bora namaanisha uchague kuku ambaye anajiuza atakapo ingia sokoni yaani kuku mwenye umbo kubwa na uzito unao takiwa. • 4. Kuandaa vifaa vya chakula na maji vya kienyeji ili kupunguza gharama za uanzishaji wa mradi. • Vifaa vya chakula na maji ni muhimu sana kwenye udhibiti wa Magonjwa ya kuku hasa yanayosambaa kupitia uchafu unaotoka kwa kuku mgonjwa. • 5.Kuandaa chakula cha kuwalisha kuku wako. • Katika suala zima la chakula na jinsi ya kuwalisha kuku wa kienyeji wengi huwa wanafanya makosa. Makosa ambayo hawapelekea kuikosa faida waliyokuwa wakitegemea kuipata wakati wa mavuno. Wengi hupata hasara kwa sababu ya gharama za chakula zinaenda juu zaidi ya faida inayopatikana. • 6. Kusanya Makoo/tetea na jogoo kwa idadi unayoweza kumudu kuwahudumia. • Nenda vijijini, kusanya Makoo/matetea na jogoo kwa idadi unayohitaji kuanza nayo. • Zingatia ubora wa kuku kama tulivyozungumza kwenye sehemu ya kwanza. • 7. Uchunguzi wa Magonjwa na tiba • Baada ya kuwafikisha kuku bandani, tenga muda wa wiki 2 za kuwachunguza ili kubaini kama wanamaambukizi yeyote ya ugonjwa. • 8. Utagaji na utamiaji wa mayai • Tengeneza viota vinavyoendana au kuzidi idadi ya tetea uliowanunua ili kuepusha kuku zaidi ya mmoja kutagia kwenye kiota kimoja, na ikitokea wametaga kiota kimoja tenganisha kila yai kiota chake. • Pia kama unaweza kutenganisha sehemu ya kulala na kutagia itakuwa ni vizuri zaidi maana kuku wanaoatamia hawata sumbuliwa. • 9. Uleaji wa vifaranga • Uleaji wa vifaranga ni kipengele muhimu sana kwenye ufugaji wa kuku. • Kuna vitu vya kuzingatia wakati wa uleaji wa vifaranga • I. Aina ya chakula unachowalisha • II. Utaratibu wa chonjo muhimu • III. Usafi wa vyombo ya chakula na maji • IV. Ukubwa wa banda uendane na idadi ya vifaranga • V. Kutibu kwa wakati mripuko wa magonjwa ya coccidiosis, pullorum, typhoid n.k • 10. Kuendeleza kizazi • Kitu muhimu ni kuhakikisha unakuza vifanga wengi ili uwe na wazazi wengi wa baadae. • Ili kuendeleza kizazi unapaswa kuhakikisha kuwa, vifaranga walionguliwa wakifisha umri wa kupandwa hawapandwi na baba au kaka zao. • • PLAYLIST • Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji • https://goo.gl/2Wkyhc • • Magonjwa ya Kuku • Bofya link kutazama video hizo • https://goo.gl/hvfVcg • • Uleaji wa vifaranga vya kuku Kwa Kutumia Brooder • https://goo.gl/xSTCfX • • Instagram • www.instagram.com/Changamkiafursatv • • What's spp • +255752209073

#############################









Content Report
Youtor.org / YTube video Downloader © 2025

created by www.youtor.org