KESHA LA ASUBUHI 16 NOVEMBER 2024 UAMSHO WA KWELI NA BANDIA











>> YOUR LINK HERE: ___ http://youtube.com/watch?v=SRlv0ge-yEs

SUBSCRIBE | COMMENT | LIKE | SHARE • UAMSHO WA KWELI NA BANDIA • Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. - Mathayo 7:16, 17. • πŸ“– Kabla ya ujio wa mwisho wa hukumu za Mungu juu ya dunia, kutakuwa, kati ya watu wa Bwana, uamsho wa utauwa wa kale ambao haujashuhudiwa tangu nyakati za mitume. Roho na uwezo wa Mungu vitamiminwa juu ya watoto wake. Wakati huo wengi watajitenga na yale makanisa ambayo upendo wa ulimwengu huu umechukua mahali pa upendo kwa Mungu na Neno Lake. Wengi, wachungaji na watu, watapokea kwa furaha kweli hizo kuu ambazo Mungu amefanya zienezwe kwa wakati huu, ili kuwaandaa watu kwa ajili ya ujio wa pili wa Bwana. Adui wa roho anatamani kuizuia kazi hii; na kabla ya wakati wa vuguvugu kama hilo kutokea, atajitahidi kuuzuia, kwa kuanzisha uamsho bandia. Katika makanisa hayo ambayo anaweza kupeleka chini ya nguvu zake za udanganyifu, atafanya ionekane kwamba baraka ya pekee ya Mungu imemiminwa; kutakuwapo na udhihirisho wa kile kinachofikiriwa kuwa ni mapenzi makubwa ya dini.... • πŸ“– Popote pale watu wanapopuuza ushuhuda wa Biblia, wakigeuka kutoka katika kweli zilizo wazi, zinazozijaribu roho zinazohitaji kujikana nafsi na kuukana ulimwengu, hapo tunaweza kuwa na uhakika kwamba baraka za Mungu hazitolewi.... • πŸ“– Dhana mbaya endelevu ya tabia, na wajibu wa sheria takatifu, vimesababisha makosa kuhusiana na uongofu na utakaso, na umesababisha kushusha kiwango cha kumcha Mungu katika kanisa. Hapa ndipo panapatikana siri ya ukosefu wa Roho na uwezo wa Mungu katika uamsho wa wakati wetu.... • πŸ”˜ Ni pale tu sheria ya Mungu inaporejeshwa kwenye nafasi yake inayofaa ndipo kunaweza kuwa na uamsho wa imani ya kale na kumcha Mungu miongoni mwa watu wanaodai kuwa watu Wake. BWANA asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu (Yeremia 6:16).

#############################









Content Report
Youtor.org / Youtor.org Torrents YT video Downloader Β© 2024

created by www.mixer.tube