SIRI YA USHINDI KWENYE VITA YA KIROHO PASTOR SUNBELLA KYANDO
>> YOUR LINK HERE: ___ http://youtube.com/watch?v=gYS7Mx3v6_0
Vazi lolote huwa linawakilisha neema ya mwenye vazi, na neema ya mtu inaweza kuwa nzito kwa mtu mwingine. Neema ya Sauli ilikua nzito sana kwa Daud. • Neema iliyokua juu ya Eliya ilikua juu ya Elisha mara baada ya Elisha kuchukua vazi la Eliya, • Sauli alitaka neema yake ndiye ikapigane na Goliathi na laiti kama Daudi angetumia neema ya Sauli na akamshinda Goliathi; • i) Utukufu wa Mungu ungegawanyishwa • ii) Vita ingepiganwa kwa namna nyingine ya kawaida • iii) Ukubwa wa muujiza ungekua umebatilishwa kutokana na namna ya kupigana. • Kuna vitu Mungu ameviacha kwenye maisha yako kwa muda, kusudi vitakapokuja kubadilishwa utukufu uwe wa Mungu peke yake! • Daudi, ilimlazimu kuingia kwenye kijito, alichukua mawe kwenye kijito, na yale mawe yalikua attached na maji.. • Sasa maji ya kile kijito ni Roho Mtakatifu na yalikupo active hakutulia mahali pamoja, hakuna mtu anaweza kukaa kwenye uwepo wa Mungu asiwe attached na Roho Mtakatifu lakini aina ya maisha inaweza kumfanya Roho Mtakatifu asiwe active kwenye maisha yako. • Kuna uwezesho unauhitaji wa kukusaidia kuvuka ulipokwama na ni aina ya uwezesho ambao huwezi kuupata sehemu yoyote tofauti na kwenye uwepo wa Mungu • Daudi alizama kwenye kijito, akachagua mawe kutoka kwenye kijito, hakuchukua tu ili mradi jiwe. Hakuchagua kuangalia ama kuzingatia ukubwa wa Goliathi alichagua kijito ambacho kulikua jawabu la changamoto yake. • Usiachague kuangalia ukubwa wa tatizo elekeza macho yako yote mahali pa suruhisho lako. • Hauwezi kufikia mwisho wa vita kama huoni umuhimu wake. Na wakati mwingine sio lazima tuwaanzishie maadui zetu vita, unasubiri waanze kama Goliathi alivyomuanza Daudi kisha wewe unawatandika, • Na unaweza kutumia silaha za maadui zako kuwamalizia kama alivofanya Daudi kwa Goliathi. • #PastorSunbella#Vita#VyaKiroho
#############################
