MWALIMU WA TAALUMA MBARONI KWA JARIBIO LA UBAKAJI
>> YOUR LINK HERE: ___ http://youtube.com/watch?v=kgzGTSlWEi8
#VIDEO: Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Msingi ya Rulanda katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera, Lameck Jonas Baikweki anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma kujaribu kumbaka mwanafunzi wa kike aliyehitimu darasa la saba mwaka huu katika shule hiyo. • Inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo alikwenda ofisini kwa Mwalimu huyo kufuatilia matokeo yake ya mtihani wa taifa, yaliyotangazwa na Baraza la Taifa la mitihani hivi karibuni. • Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Kamishina Msaidizi Mwandamizi Blasius Chatanda, amesema alikamatwa akiwa kwenye harakati za kumbaka mwanafunzi huyo huku akimpaka mafuta kwenye sehemu za siri ndipo watu walisikia purukushani na wakavamia ofisi hiyo na kufanikiwa kumnusuru mwanafunzi huyo.
#############################
