CHACHA ARIPOTI KAZINI TABORA AJITAMBULISHA KAMA MCHAPAKAZI AKUMBUSHIA KESI YA MAUJI KALIUAA
>> YOUR LINK HERE: ___ http://youtube.com/watch?v=PfXBIU5GOMI
#CgOnlineTv • Mkuu mpya wa mkoa wa Tabora Paul Matiko Chacha ameripoti kazini leo na kuahidi kusimamia haki, usalama na maendeleo ya wananchi wa mkoa wa Tabora. • Akizungumza katika kikao cha kukaribishwa kazini mkuu wa mkoa wa Tabora Paul Chacha amesema moja ya vipaumbele vyake ni usalama akitolea mfano kesi ya mauaji ambayo aliiacha miaka miwili iliyopita alipokua mkuu wa wilaya ya Kaliua ambapo mwanaume mmoja alituhumiwa kuwaua watoto wawili wa mke wake na kuwazika ndani kisha kutokomea kusikojulikana na kuliagiza jeshi la polisi kumsaka na kumkamata mtuhumiwa huyo. • Chacha amejitambulisha kama mtu mwenye msimamo, muumini wa haki na kuahidi kwamba katika kusimamia haki na maendeleo ya mkoa wa Tabora Kwa kushirikiana na viongozi na wananchi wa halmashauri zote za mkoa huo. • Awali akimkaribisha mkuu wa mkoa Katibu tawala wa mkoa wa Tabora Dkt. John Mboya ameahidi ushirikiano Kwa niaba ya watumishi wengine wa mkoa akisema kwamba mkoa una watumishi waadilifu na wachapa kazi ambao watamsaidia kutimiza majukumu yake mapya kama mkuu wa mkoa. • Kwa upande wake Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Tabora Ramadhani Kapela akishukuru kwa niaba ya wenyeviti wa halmashauri za mkoa wa Tabora amesema ni matumaini ya wengi kwamba atautumikia mkoa wa Tabora kwa ufanisi kwakua yeye si mgeni katika mkoa huo. • Mkuu wa mkoa mpya Paul Matiko Chacha anachukua nafasi ya aliyekua mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Burian aliyehamishiwa mkoani Tanga katika mabadiliko yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu siku chache zilizopita. • #CgOnlineUpdates
#############################