WASTARA Amlilia SAJUKI Aandika Ujumbe Mzito
>> YOUR LINK HERE: ___ http://youtube.com/watch?v=z1yzrycGi5U
WASTARA Amlilia SAJUKI, Aandika Ujumbe Mzito! • Ni miaka kadhaa imepita tangu aliyekuwa muigizaji maarufu Bongo, Juma Kilowoko 'Sajuki' afariki dunia na kumuacha mkewe ambaye pia ni muigizaji Wastara akiwa na mtoto mmoja anayeitwa Farheen. • Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wastara ameandika ujumbe mzito unaomuhusu mumewe huyo. • Najua kuwa ni dhambi kukupost ni dhambi kuomboleza lakini nitasahau vipi hii siku kibaya zaidi kila unapoingia mwaka mpya • Uliponiona alfajiri nimesimama pembeni yako tukiwa hospital ya Muhimbili Uliniambia nashukuru na mimi nimeona mwaka mwingine hata nikifa kesho mtasema alikufa mwaka mpya. • Halafu ukasema kilichobadilika ni namba tu mke wangu mambo yote yapo vilevile yalivyopangwa yawe yatakuwa hapo ukaanza kuniulizia muda kila wakati unauliza saa ngapi wenzangu wote waliokuwepo walijua kuwa unakufa mimi peke yangu nilizibwa ufahamu sikujua maskini ilipofika saa 10 jioni ukaniita uninong'oneze kitu ukaniiimbia sikion halafu ukasema nenda nje kajirecord na simu huu wimbo ili usisahau maana sitakuwepo tena! • Nikahamaki sana ukasema mke wangu naogopa kukwambia ukweli lakini kubali tu kuwa mimi ninakufa nakuacha maskini peke yako watakutesa tu binaadamu, Daah nilidhani meneno ya mgonjwa kumbe asubuhi ya tarehe 2 nilikuta umeshazungushiwa pazia za kijani ambazo toka siku hiyo sizipendi nikiziona natamani kuzichanachana, MUNGU aliye juu ndiye anaejua ukweli wa moyo wangu hakuna kiumbe yoyote hapa duniani atakaeusemea moyo wangu. • Hata niolewe mara 10000000 lakini wewe ulifungua ukurasa wa upendo wa kweli na hakuna atakaenizuia kukuenzi na kukuombea mpaka nakufa japo mashetani yapo kuukana ukweli huu ila hawatanizuia nafsi yangu...MUNGU AKUPE NURU KWENYE KABURI LAKO AMIIN Ameandika Wastara • #RIPSAJUKI • Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: • www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho USIKUBALI KUPITWA NA HII, BONYEZA LINK https://www.youtube.com/watch?v=L4UGw.
#############################
New on site